Verse 1
Kama ni mapenzi
ya kuniudhi kila saa
ya kunifanya mi kulia
na kama huridhiki
na mbona hujasema
ili niweze rekebisha
nifanye mambo shwari
nikiamini u kwangu
na kukusifu kwa wazazi
hujali tenda hisia zangu
sijui tunapokwenda
lakini najua tulipotoka
kutoka sitoki nimetekwa nyara
kukuwacha siwezi kibarua ngumu
nashindwa ni nini ntafanya uridhike
nimetekwa ndani
mtandao wa mapenzi
basi nakuomba
uniteke tu bila mateso
Chorus
tazama, nimezama
ndani ya bahari
la penzi lako
siwezi
kusonga mbele
kurudi nyuma
sijielewi
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama wanipenda
jaribu kunipa raha
Verse 2
mi nashangaa
watu wakisema
eti tunapendana
japo tunazozana
ni vizuri mami
nyumba kuwa na siri
lakini jaribu
tusuluhishe
bila hivyo
itakuwa mchezo
wa kuigiza
kwenye mambo bandia
mimi sitaki
mambo ya kujifanya
ati tunapendana
tena tunatesana
nimejaribu sana kujitoa ndani
kila nikipanga napangua mwenyewe
natamani sana ungeelewa hivyo
mimi mateka
mimi pumbavu
wa penzi lako
nieleze ni lini ntakuwa huru
Chorus
tazama, nimezama
ndani ya bahari
la penzi lako
siwezi
kusonga mbele
kurudi nyuma
sijielewi
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama wanipenda
jaribu kunipa raha
Verse 3
jaribu baby
mambo
ya kunifanya kumbafu haifai
mambo yo yo yo yo yo
haifai
jaribu baby
tusuluhishe
nimejaribu sana kujitoa ndani
kila nikipanga napangua mwenyewe
natamani sana ungeelewa hivyo
mimi mateka
mahabusu
wa penzi lako
nieleze ni lini ntakuwa huru
Chorus
tazama, nimezama
ndani ya bahari
la penzi lako
siwezi
kusonga mbele
kurudi nyuma
sijielewi
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama unanipenda
jaribu kunipa raha